Jarida la Mapishi

Supu ya kuku

Supu ya kuku | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1
  • Walaji
    4

Supu ya kuku, ni supu tamu yenye krimu, ambayo hupikwa kwa kuchemsha nyama ya kuku, mtindi, tui la nazi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Supu hii yafaa kula majira ya jioni kabla ya chakula cha jioni, katika kipindi cha msimu wa vuli, pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya kuku.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, vipande vya nyama ya kuku, maji, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 45, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani, tangawizi, majani ya mvuje, mbegu za giligilani, pamoja na binzari nyembamba, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step4

    Weka mtindi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vyema na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye sufuria lenye supu, kisha koroga vizuri.

    Step5

    Ongeza moto na uweke moto mkubwa, kisha acha ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.

    Step7

    Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5. Epua na uweke pembeni kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step8

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka binzari nyembamba kwenye hilo sufuria, kisha koroga vizuri. Epua na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.