Jarida la Mapishi

Supu ya nyanya na choroko

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Supu ya nyanya na choroko, ni supu tamu ambayo hunywewa zaidi katika kipindi cha baridi, hasa kutokana na choroko kuwa na protini kwa wingi ambayo husaidia kuongeza joto mwilini. Supu hii yafaa kunywa kwenye majira ya jioni kabla ya mlo wa jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya nyanya na choroko.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, majani ya giligilani, choroko, vitunguu swaumu, vitunguu maji, viazi mviringo, pilipili manga, chumvi, nyanya, karoti, maji, pamoja na maharage machanga, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kichemka kwa muda wa dakika 35, au hadi utakapo ona choroko pamoja na maharage machanga vimeiva. Epua supu na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka supu uliyo ichemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step4

  Rudisha supu kwenye sufuria, kisha weka tena ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 7 mpaka 10. Epua supu na umimine kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

  Step5

  Chukua sufuria ndogo yenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acja mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mbegu za giligilani pamoja na binzari nyembamba, kisha kaanga kwa sekunde kadhaa. Epua viungo hivyo na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *