Jarida la Mapishi

Supu ya kamba

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Supu ya kamba, ni supu tamu sana yenye nyanya, inayopikwa kwa kutumia kamba wabichi, tui la nazi pamoja na limao. Supu hii yafaa kunywa wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya kamba.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maboga, kamba, vikombe 5 vya maji, vitunguu swaumu, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona kamba wamebadilika rangi na kuwa na rangi ya pinki, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Chukua kamba waliomo kwenye sufuria, kisha ondoa magamba, mshipa wa katikati, pamoja na mikia yao.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka vitunguu maji kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa vitunguu maji hivyo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uviweke pembeni kwenye kontena.

  Step5

  Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena jingine.

  Step6

  Weka kamba kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona kamba hao wamesagika. Ondoa kamba hao kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke kwenye sufuria lenye supu.

  Step7

  Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji ulivyo visaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step8

  Weka mbegu za giligilani pamoja binzari ya manjano, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi.

  Step9

  Weka mchanganyiko wa nyanya ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye supu.

  Step10

  Weka pia limao pamoja na tui la nazi kwenye hilo sufuria lenye supu halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step11

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *