Jarida la Mapishi

Supu ya nyanya na mboga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  6

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, jani la mbei, binzari nyembamba, pamoja na liki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona mashina ya liki zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step2

  Weka vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na mashina ya figili, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

  Step3

  Weka mbegu za giligilani pamoja na mboga, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10. Epua mchanganyiko huu na uweke kwenye kontena.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step5

  Ondoa mchanganyiko huo wa nyanya kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kikaango ulichotumia kukaanga mboga. Weka chumvi pamoja na pilipili manga, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step6

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani. Weka maji, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.

  Step7

  Weka mchanganyiko wa mboga uliomo kwenye kontena na uchanganye vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi. Epua na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *