Jarida la Mapishi

Supu ya karoti

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 30
 • Walaji
  4

Supu ya karoti, ni supu nzuri ambayo mtu yoyote anayependa karoti ataipenda. Supu hii iliyo sheheni ladha ya karoti inapikwa kwa kutumia karoti zilizokunwa pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu ya karoti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka majani ya mbei, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step2

  Weka tangawizi na uendelee kukaanga kwa muda wa dakika 1 zaidi.

  Step3

  Weka karoti pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona karoti zimeiva.

  Step4

  Weka vikombe 5 vya maji pamoja na chumvi, kisha acha ichemke katika moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step5

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Ondoa majani ya mbei kwenye sufuria na uyaweke pembeni. Mimina supu kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona supu imesagika vyema na kuwa laini.

  Step6

  Rudisha supu uliyoisaga kwenye sufuria, kisha acha ichemke hadi utakapo ona supu imepungua kwa kiwango cha ¼.

  Step7

  Weka kikombe 1 cha maji kwenye supu, kisha acha ichemke tena. Ukiona supu imeanza kuchemka, mimina mtindi huku ukikoroga, kisha acha iendelee kuchemka, hadi utakapo ona supu imechemka vizuri.

  Step8

  Weka limao pamoja na pilipili manga, halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *