Jarida la Mapishi

Supu ya nyanya

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  6

Supu ya nyanya, ni supu tamu yenye krimu, inayopendwa sana kunywewa na watu wakati wa kipindi cha kiangazi. Supu hii inakuwa tamu zaidi endapo itapikwa kwa kutumia nyanya nzuri na zilizo iva vizuri. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika supu hii ya nyanya.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step2

  Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena.

  Step4

  Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, karoti pamoja na viazi mviringo, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena jingine.

  Step5

  Weka pia nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona nyanya hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.

  Step6

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye kwenye hilo sufuria vitunguu maji pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step7

  Weka mchanganyiko wa karoti ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step8

  Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka nyanya ulizo zisaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

  Step9

  Weka maji, chumvi, pamoja na sukari, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke.

  Step10

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, kisha epua na uweke pembeni ipoe.

  Step11

  Chukua chujio. Chuja supu kwenye kontena safi, kisha mimina supu uliyo ichuja kwenye sufuria uliyotumia kupikia supu.

  Step12

  Rudisha sufuria lenye supu kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha ichemke.

  Step13

  Chukua kikombe chenye maziwa. Weka unga wa mahindi ndani ya hicho kikombe chenye maziwa halafu koroga vizuri, kisha mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye supu.

  Step14

  Weka binzari nyembamba pamoja na kungumanga halafu koroga vizuri, kisha epua na umimine kwenye kontena.

  Step15

  Mimina mtindi ya hilo kontena, halafu koroga vizuri, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *