Jarida la Mapishi

Supu ya spinachi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Supu ya spinachi kama jina lake lilivyo, ni supu inayopikwa kwa kutumia mboga ya spinachi kama kiungo kikuu. Supu hii ni tamu, yenye virutubisho vingi na rahisi sana kupika ambayo unaweza kuipika katika muda mfupi sana wa ndani ya dakika 30 tu. Waweza kunywa supu hii pamoja na chakula cha mchana, au kama starter ya chakula cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya spinachi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hiyo sufuria, mboga ya spinachi, majani ya giligilani, majani ya minti, vitungu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko uliochemsha, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria nyingine kubwa yenye mafuta ya kupikia na uiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye unga wa ngano kwenye hilo sufuria na ukaange huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona unga umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Mimina maziwa taratibu kwenye hilo sufuria huku ukikoroga. Mimina pia na mchanganyiko wa spinachi uliousaga huku ukiendelea kukoroga.

  Step6

  Weka garam masala na ukoroge vizuri, kisha mimina mtindi na ukoroge tena vizuri. Epua supu hiyo na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *