Jarida la Mapishi

Supu ya tangawizi

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Supu ya tangawizi, ni supu tamu yenye harufu nzuri ya tangawizi. Kwa kawaida supu hii hupikwa kwa kutumia tangawizi pamoja na viungo kama vile; binzari ya manjano, vitunguu swaumu, pamoja na viungo vingine vingi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya tangawizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka ½ kikombe cha maji, kisha roweka mbaazi ndani ya hilo bakuli lenye maji, kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbaazi ulizo ziroweka pamoja na maji yake, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za pilipili manga, pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria mchanganyiko ulio usaga, maji, pamoja na chumvi, kisha weka kwenye sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha ichemke.

  Step4

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, kisha epua na uweke kwenye kontena.

  Step5

  Chukua sufuria ndogo yenye mafuta ya kupikia, na uiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *