Jarida la Mapishi

Supu ya dengu

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Supu ya dengu, ni supu rahisi kupika na yenye afya ambayo hupikwa kwa kutumia nafaka ya dengu pamoja na viungo. Supu hii yafaa sana kunywa nyakati za jioni pamoja na chakula cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya dengu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka maji kiasi, kisha roweka dengu ndani ya hilo bakuli lenye maji, kwa muda wa saa 24. Baada ya saa 24, mwaga maji yote yaliyomo kwenye hilo bakuli, na kubakiwa na dengu peke yake.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, dengu, vikombe 6 vya maji, mdalasini, iliki, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na chumvi, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona dengu zimeiva.

  Step3

  Weka tomato sauce na ukoroge vizuri, kisha acha ichemke katika moto mkubwa huku ukikoroga mara kwa mara, kwa muda wa dakika 5.Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa saa 1.

  Step4

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step5

  Weka nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo, hadi utakapo ona nyanya zimeiva na kuwa laini.

  Step6

  Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye sufuria lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *