Jarida la Mapishi

Supu ya choroko

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Supu ya choroko, ni supu tamu ambayo inasaidia sana katika kuboresha afya. Supu hii hupikwa kwa kitumia choroko pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile; binzari ya manjano, binzari nyembamba na tangawizi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya choroko.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka kikombe 1 cha maji, kisha roweka choroko ndani ya hilo bakuli lenye maji, kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Baada ya dakika 30, mimina choroko hizo zilizo rowekwa kwenye sufuria kubwa. Weka pia kwenye hilo sufuria, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na vikombe 2 vya maji, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha ichemke.

  Step3

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona choroko zimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa choroko ulio chemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step5

  Mimina mchanganyiko wa choroko ulio usaga kwenye lile sufuria kubwa ulilotumia kuchemsha mchanganyiko huo wa choroko. Weka tangawizi pamoja na vikombe 4 vya maji, kisha funika sufuria na acha ichemke katika moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5.

  Step6

  Chukua sufuria nyingine ndogo lenye mafuta ya kupikia na uweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mbegu za haradali, binzari nyembamba, pilipili manga pamoja na majani ya mvuje, halafu kaanga kwa muda wa sekunde 30, kisha epua mchanganyiko huo na umimine kwenye sufuria lenye supu.

  Step7

  Weka limao pamoja na majani ya giligilani, halafu koroga vizuri. Acha supu ichemke kwa muda mfupi, kisha epua na upakue kwenye bakuli tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Ali Hamad

   Giligilani siijui na haradali sizijui

   • Mary Joachim

    Viungo vyote vilivyoandikwa humu vinapatikana kwenye masoko yote makubwa. Ukienda sokoni, nenda kaulizie kwenye maduka yanayouza viungo.

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *