Jarida la Mapishi

Saladi ya mayai

Saladi ya mayai | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Saladi ya mayai, ni saladi tamu inayo tengenezwa kwa kutumia mayai yaliyo chemshwa. Saladi hii yaweza kuliwa pamoja na mkate au sandwich. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya mayai.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Ondoa mbegu hizo za ufuta mweupe kwenye kikaango, na uziweke pembeni kwenye bakuli.

    Step2

    Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye kikaango hicho hicho, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step3

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step4

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mayai pamoja na maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step5

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 12.

    Step6

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na mayai peke yake, kisha acha yapoe.

    Step7

    Menya maganda ya mayai hayo, kisha yakate kate.

    Step8

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mayai uliyo yachemsha, majani ya giligilani, chumvi, Yogurt Cheese, mbegu za ufuta, tangawizi, curry powder, pamoja na binzari nyembamba, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.