Jarida la Mapishi

Saladi ya nyanya za kijani

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Saladi ya nyanya za kijani, ni saladi ambayo hutengenezwa kwa kutumia nyanya ambazo hazijaiva. Utamu wa saladi hii upo kwenye ladha ya kipekee ya nyanya hizi za kijani ambayo ni nusu utamu na nusu ubichi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya nyanya za kijani.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka nyanya kwenye hicho kikaango na uzisambaze vizuri.

  Step2

  Nyunyizia mafuta kupikia juu ya hizo nyanya, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4.

  Step3

  Nyunyizia mbegu za giligilani pamoja chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona nyanya hizo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step4

  Weka limao pamoja na majani ya giligilani, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na upakue kwenye chombo safi.

  Step5

  Nyunyizia Chaat Masala na uchanganye vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *