Jarida la Mapishi

Saladi ya dengu

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Saladi ya dengu, ni saladi iliyo sheheni virutubisho vya protini kwa wingi. Saladi hii ni rahisi sana kutengeneza na inatengezwa kwa kutumia dengu pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya dengu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, nyanya, tango, vitunguu vya kijani, ¼ kikombe cha majani ya giligilani pamoja na ½ kijiko cha Chaat Masala, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step3

  Weka mbegu za giligilani, vijiko 1½ vya chai vya Chaat Masala iliyobakia, pamoja na ¼ kikombe cha majani ya giligilani yaliyobakia, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step4

  Weka dengu, maji, pamoja na Tamarind Paste, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona maji kwenye sufuria yamekauka, kisha epua na uweke pembeni.

  Step5

  Weka mchanganyiko huu kwenye kontena lenye mchanganyiko ulio changanya mwanzoni pamoja na mbegu za komamanga, kisha changanya vizuri, halafu acha ipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *