Jarida la Mapishi

Saladi ya maharage

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Saa 1
 • Walaji
  4

Saladi ya maharage, ni saladi nzuri inayo tengenezwa kwa kutumia maharage mekundu pamoja na viungo. Saladi hii yafaa sana kuliwa pamoja na nyama choma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya maharage.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka vikombe 2 vya maji, kisha roweka maharage ndani ya hilo bakuli lenye maji kwa muda wa saa 24.

  Step2

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango mbegu za binzari nyembamba, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili zipoe.

  Step3

  Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

  Step4

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maharage uliyo yaroweka na maji yake, vitunguu swaumu, iliki, mdalasini, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step5

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache ichemke muda wa saa 1, au hadi utakapo ona maharage yameiva. Epua maharage hayo na uyaweke kwenye kontena.

  Step6

  Chukua kontena jingine dogo. Weka ndani ya hilo kontena, binzari nyembamba, mtindi, Tamarind Paste, tangawizi, pamoja na Chaat Masala, kisha changanya vizuri. Weka mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye maharage, pamoja na majani ya minti na majani ya giligilani, kisha changanya vizuri tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *