Jarida la Mapishi

Saladi ya viazi mviringo

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  4

Saladi ya viazi mviringo, ni aina ya saladi ambayo asili yake ni kutoka nchini India. Saladi hii hutengezwa kwa kutumia viazi mviringo pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya viazi mviringo.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango na ukaange bila kuweka mafuta kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili zipoe.

  Step2

  Chukua kinu. Weka mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga ndani ya hicho kinu, kisha twanga hadi utakapo ona zimesagika vizuri.

  Step3

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, viazi mviringo pamoja na maji ya kutosha, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimeiva. Epua na uweke pembeni ili vipoe. Viazi vikisha poa, vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step4

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, ¼ kijiko cha chai cha chumvi, pilipili manga, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha changanya vizuri.

  Step5

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi ulivyo vichemsha kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.

  Step6

  Weka tangawizi, majani ya giligilani pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huo na uweke kwenye bakuli kubwa.

  Step7

  Weka kwenye hilo bakuli lenye viazi, mchanganyiko wa mtindi pamoja na binzari nyembamba, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *