Jarida la Mapishi

Saladi ya viazi na njegere

Saladi ya viazi na njegere | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    4

Saladi ya viazi na njegere, ni saladi ya kipekee ambayo hutengezwa kwa kutumia, viazi mviringo, viazi vitamu, njegere, vitunguu maji, viungo, pamoja na ukwaju. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya viazi na njegere.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua sufuria jingine kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi vitamu pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step5

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step6

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step7

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, viazi mviringo pamoja na viazi vitamu ulivyo vichemsha, kisha kaanga huku ukivigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa viazi hivyo kwenye kikaango na uviweke pembeni kwenye sahani, kisha acha vipoe.

    Step8

    Weka njegere kwenye kikaango hicho hicho, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona zimeanza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step9

    Weka mchanganyiko wa viazi mviringo na viazi vitamu ulivyo vikaanga, Tamarind Paste, chumvi, Chaat Masala, pamoja na majani ya giligilani, halafu kaanga huku ukivigeuza viazi mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni kwenye chombo safi.

    Step10

    Nyunyizia vitunguu maji, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.