Jarida la Mapishi

Saladi ya kunde

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Saa 1
 • Walaji
  4

Saladi ya kunde, ni saladi yenye afya isiyokuwa na gluteni. Saladi hii ni rahisi sana kutengeneza, na hutengenezwa kwa kutumia kunde, viazi mviringo, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya kunde.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli la ukubwa wa wastani. Weka vikombe 2 vya maji, kisha roweka kunde ndani ya hilo bakuli lenye maji kwa muda wa saa 24.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, kunde ulizo ziroweka pamoja na maji yake, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step3

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona kunde zimeiva, kisha epua na uweke pembeni.

  Step4

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, kunde ulizozichemsha pamoja na nyanya, vitunguu vya kijani, tangawizi, majani ya minti, pamoja na limao halafu koroga vizuri, kisha acha mchanganyiko huo upoe. Ukiona mchanganyiko huo umepoa, mimina mtindi na ukoroge tena vizuri.

  Step5

  Chukua sufuria ndogo yenye mafuta ya kupikia na uiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa kunde, kisha changanya vizuri.

  Step6

  Weka pia kwenye hilo kontena mboga ya lettuce, pamoja na Chaat Masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *