Jarida la Mapishi

Saladi ya kabichi na limao

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  4

Saladi ya kabichi na limao, ni saladi nzuri na rahisi kutengeneza. Saladi hii hutengenezwa kwa kutumia kabichi mbichi iliyo katwa katwa na kuchanganywa pamoja na limao. Saladi hii yafaa kuliwa pamoja na samaki au nyama ya ng’ombe ya kuchoma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya kabichi na limao.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za haradali, binzari nyembamba, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa sekunde kadhaa.

  Step2

  Weka kabichi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona kabichi imeanza kunyauka. Epua mchanganyiko huu na uweke kwenye kontena kubwa.

  Step3

  Weka limao pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Schomiq

   Safi Sana.

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *