Jarida la Mapishi

Saladi ya spinachi

Saladi ya spinachi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    4

Saladi ya spinachi, ni moja ya saladi tamu na maarufu sana duniani. Saladi hii hutengenezwa kwa kutumia mboga ya spinachi mbichi, nyanya, pamoja na viungo vingine. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya spinachi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua kontena kubwa. Weka spinachi ndani ya hilo kontena, kisha weka pembeni.

    Step4

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, tangawizi, limao, pamoja na asali, halafu koroga vizuri, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step5

    Weka mtindi, binzari nyembamba uliyo ikaanga, chumvi, pamoja na pilipili manga, halafu koroga vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye kontena lenye spinachi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.