Jarida la Mapishi

Saladi ya matango na karanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 1
 • Walaji
  4

Saladi ya matango na karanga, ni saladi tamu ambayo hutengenezwa kwa kutumia matango yaliyo katwa katwa, karanga zilizo kaangwa, pamoja na viungo. Saladi hii yafaa kula katika msimu wa kiangazi, pamoja na chakula chochote ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya matango na karanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena matango, karanga, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua sufuria ndogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mbegu za haradali, curry powder, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde kadhaa.

  Step3

  Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye kontena lenye saladi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *