Jarida la Mapishi

Pilau ya spinachi

Pilau ya spinachi | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Pilau ya spinachi, ni chakula kizuri na chenye afya ambacho hupikwa kwa kutumia pilau ya binzari nyembamba, pilipili hoho, spinachi, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya spinachi.

Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika pilau ya binzari nyembamba ambayo itatumika kwenye pishi hili.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, vitunguu swaumu, majani ya uwatu, pamoja na spinachi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona spinachi imenyauka.

  Step2

  Weka pilipili hoho, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona pilipili hoho imeiva.

  Step3

  Weka chumvi, kisha koroga vizuri.

  Step4

  Weka pilau ya binzari nyembamba, Chaat Masala, pamoja na garam masala halafu changanya vizuri. Funika sufuria hilo vizuri, kisha epua na uweke pembeni.

  Step5

  Acha pilau itulie kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, kisha pakua kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.