Jarida la Mapishi

Pilau ya kamba

Pilau ya kamba | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Pilau ya kamba, ni chakula kitamu kinachopikwa kwa kutumia kamba wadogo wabichi, mchele pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya kamba.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step2

    Weja majani ya giligilani pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona majani ya giligilani yamenyauka.

    Step3

    Weka kamba, mbegu za kisibiti, garam masala, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona kamba wamebadilika rangi na kuwa na rangi ya pinki.

    Step4

    Mimina tui la nazi na ukoroge vizuri, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni.

    Step5

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena wali wa binzari ya manjano uliopikwa pamoja na mchuzi wa kamba.

    Step6

    Nyunyizia limao halafu changanya vizuri, kisha funika kontena na uache wali utulie kwa muda wa dakika 5, kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.