-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 55
-
Walaji4
Kuku wa spinachi, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, spinachi, vitunguu maji, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari ya manjano au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa spinachi.
Ingredients
Directions
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, mtindi, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya minti, majani ya uwatu, garam masala, kungumanga, chumvi, pamoja na kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.
Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka spinachi kisha koroga vizuri. Funika sufuria kisha pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona spinachi imenyauka. Kumbuka kukoroga mara 1 au 2 wakati unapika.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka mchanganyiko wa kuku, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva.
Mimina maziwa halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 2. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review