Jarida la Mapishi

Pilau ya binzari nyembamba

Pilau ya binzari nyembamba | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Pilau ya binzari nyembamba, ni chakula kitamu ambacho chaafaa kuliwa pamoja na mboga au kitoweo chochote kile ukipendacho, iwe ni mchuzi wa nyama ya ng’ombe, mchuzi wa kuku, au hata mboga ya spinachi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya binzari nyembamba.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, pilipili manga, mchele, pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele.

    Step3

    Weka chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step5

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.