-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Mchuzi wa nyama ya kusaga na viazi, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia, nyama ya kusaga, vitunguu maji, viazi mviringo, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari ya manjano, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya kusaga na viazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, ¼ kijiko cha chai cha iliki, mdalasini, majani ya mbei, binzari nyembamba, viazi, nyama ya kusaga, nyanya, majani ya giligilani, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10.
Weka mbegu za giligilani, garam masala, mbegu za uwatu, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina mtindi halafu funika sufuria, kisha acha ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na mchuzi umekuwa mzito.
Weka ½ kijiko cha chai cha iliki iliyobaki halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review