Jarida la Mapishi

Wali wa viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  4

Wali wa viazi, ni chakula rahisi sana kupika ambacho unaweza kukipika kwa muda mfupi sana wa ndani ya dakika 30 tu. Wali huu hupikwa kwa kutumia mchele, viungo pamoja na viazi mviringo au viazi vitamu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa viazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria dogo. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step2

  Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

  Step3

  Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step4

  Chukua kikaango kikubwa na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka nazi kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka tangawizi halafu endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi, kisha epua na uweke pembeni.

  Step6

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kiaha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za haradali, mbegu za uwatu, viazi mviringo, majani ya giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

  Step7

  Weka wali mweupe pamoja na mtindi halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mtindi wote umekauka.

  Step8

  Epua wali na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *