Jarida la Mapishi

Samaki wa kuchoma

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Samaki wa kuchoma, ni samaki mtamu na mwenye ladha ya kipekee ambaye huandaliwa kwa kuchanganywa pamoja na viungo, kisha kuchomwa kwenye jiko la kuchomea nyama. Samaki huyu anafaa sana kuliwa pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsj ya kupika samaki huyu wa kuchoma.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mafuta ya kupikia, mbegu za kisibiti, chumvi, tangawizi, vitunguu swaumu, tui la nazi, binzari nyembamba, pamoja na limao, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka minofu ya samaki, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona minofu yote ya samaki imeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.

  Step3

  Washa jiko la kuchomea nyama na upake mafuta juu ya wavu wa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka vipande vya minofu ya samaki juu ya hilo jiko la kuchomea nyama, na uchome huku ukivigeuza kwa muda wa 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona minofu hiyo ya samaki imeiva.

  Step4

  Ondoa minofu hiyo ya samaki kutoka kwenye jiko la kuoka na uiweke kwenye sahani. Nyunyizia Chaat Masala juu ya hiyo minofu ya samaki, kisha weka mezani tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *