Jarida la Mapishi

Kahawa ya viungo

Kahawa ya viungo | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  2

Kahawa ya viungo, ni kinywaji ambacho hupikwa kwa kuchemsha kahawa pamoja viungo vya aina mbali mbali kama vile, iliki, mdalasini, karafuu na tangawizi. Kahawa hii yafaa kunywa pamoja na kitafunio chochote ukipendacho hasa katika kipindi cha msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza kahawa hii ya viungo.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maji, mdalasini, karafuu, pamoja na iliki, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka hadi utakapo ona maji yamepungua kiwango na kuwa ¾, na yaliyobaki yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step2

  Weka kahawa na ukoroge vizuri, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka katika moto wa wastani kwa muda wa dakika 1 zaidi.

  Step3

  Epua kahawa na uweke pembeni ili ipoe. Ukiona imepoa, iweke kwenye friji ili ipate baridi kwa muda wa saa 2 mpaka siku 2.

  Step4

  Baada ya saa 2 au siku 2, ondoa kahawa hiyo kwenye friji na uichuje kwenye vikombe 2. Weka maziwa kwenye hivyo vikombe, kisha ukoroge vizuri, tayari kwa kunywa.

  Conclusion

  Kahawa hii yafaa kunywa ikiwa ya baridi. Tafadhali, usipashe moto kahawa hii baada ya kuitoa kwenye friji. Waweza kuweka sukari kadiri ya mahitaji yako kwenye kahawa hii ukipenda.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.