Jarida la Mapishi

Chai ya shamari na iliki

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  2

Chai ya shamari na iliki, ni chai nzuri sana ambayo inasaidia mtu ambaye amevimbiwa na tumbo la chakula. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza chai hii ya shamari na iliki.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maji, iliki, pamoja na mbegu za shamari, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu, hadi utakapo ona maji yamebadilika rangi na kupungua kwa kiwango cha ⅓.

  Step3

  Weka majani ya chai halafu koroga vizuri, kisha zima jiko na uache chai itulie kwa muda wa dakika 2.

  Step4

  Mimina maziwa halafu koroga vizuri, kisha washa tena jiko na uache ichemke.

  Step5

  Ukiona imechemka, zima jiko, kisha epua na uweke pembeni.

  Step6

  Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Chuja chai ndani ya hivyo vikombe. Weka sukari kadiri ya mahitaji yako, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *