Jarida la Mapishi

Lemonade ya rosemary

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Lemonade ya rosemary, ni kinywaji ambacho kitashangaza watu wengi wanao ufahamu mmea wa rosemary. Najua hapo ulipo unawaza kichwani mwako, rosemary kwenye lemonade? Ndio. Majani ya rosemary, husaidia kuyafanya malimao yawe na ladha nzuri zaidi. Ikiwa wewe ni mpenzi wa mmea wa rosemary, basi nakuhakikishia utaipenda lemonade hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya rosemary.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, majani ya rosemary, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.

  Step3

  Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *