Jarida la Mapishi

Smoothie ya lozi na blueberry

 • Maandalizi
  Dakika 5
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Smoothie ya lozi na blueberry, ni smoothie tamu iliyo sheheni virutubisho vya Protini kwa wingi, ambayo hutengengezwa kwa kutumia lozi zilizo sagwa, matunda ya blueberry, maziwa, pamoja na mtindi. Smoothie hii yafaa kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kinywaji cha kawaida wakati wowote pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho.Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza smoothie ya lozi na blueberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, matunda ya blueberry, mtindi, lozi, maziwa, mbegu za ngano, pamoja na asali, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Mimina smoothie kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *