Jarida la Mapishi

Biskuti za vanilla

Biskuti za vanilla | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 45
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    30

Biskuti za vanilla, ni biskuti zenye ladha tamu ya vanilla ambayo wakati mwingine ladha hii huonekana kama ladha ya kawaida tu. Biskuti hizi sio tu ni rahisi kutengeneza, pia unaweza kuzipika biskuti hizi bila kuhangaika. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsj ya kupka biskuti hizi za vanilla.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi pamoja na sukari kisha changanya vizuri hadi utakapo ona sukari imechanganyika vyema pamoja na siagi.

    Step2

    Weka yai pamoja na vanilla extract, na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, unga wa mahindi pamoja na chumvi, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.