-
MaandaliziSaa 1 Dk.16
-
KupikaDakika 14
-
Walaji30
Biskuti za blueberry, ni biskuti rahisi sana kupika ambazo hupikwa kwa kutumia matunda halisi ya blueberry, maziwa, maganda ya limao, pamoja na vanilla extract. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi blueberry.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, maziwa, maganda limao, na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, chumvi, baking soda, pamoja na matunda ya blueberry, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 14, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review