-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji4
Mayai ya kuvuruga yenye vitunguu, ni chakula kizuri ambacho chafaa kuliwa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, wakati wa chakula cha mchana au wakati wa chakula cha jioni. Vitunguu vinavyowekwa, hufanya mayai haya yawe matamu na yenye ladha ya kipekee zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mayai haya ya kuvuruga yenye vitunguu.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mayai, chumvi, pamoja na pilipili manga, kisha piga piga mchanganyiko huo vizuri.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.
Weka mchanganyiko wa mayai, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.
Weka majani ya giligilani, halafu endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi, au hadi utakapo ona yameiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review