Jarida la Mapishi

Vimanda vya ukwaju

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  4

Vimanda vya ukwaju, ni kitafunio kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mayai yaliyo changanywa na ukwaju pamoja na viungo. Vimanda hivi vyafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi pamoja na chai au kahawa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika vimanda hivi vya ukwaju.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mayai, majani ya giligilani, pilipili hoho, pilipili manga, chumvi, vitunguu swaumu, Tamarind Paste, tangawizi, sukari, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step3

  Weka mchanganyiko wa mayai uliochanganya, kisha funika kikaango na ukaange kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona upande wa chini wa mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. (Weka mchanganyiko huo kwa awamu 2)

  Step4

  Telezesha kimanda kwenye sahani kubwa. Weka kijiko cha kukaangia juu ya kimanda na ukishikilie vizuri, kisha pindua sahani juu chini ili kimanda kipate kugeuka.

  Step5

  Rudisha kimanda kwenye sahani, kisha itelezeshe kwenye kikaango. Kaanga upande huo mwingine wa kimanda hicho kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona na upande huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Kunja kimanda hicho katikati, kisha epua na uweke kwenye sahani, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *