Jarida la Mapishi

Bisi za maboga

Bisi za maboga | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  10

Bisi za maboga, ni bisi ambazo hupikwa kwa kutumia boga lililo sagwa pamoja na viungo. Bisi hizi zafaa kula kama kitindamlo au kama kitafunio cha kawaida, hasa wakati ambao unatizama filamu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika, bisi hizi za maboga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Washa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 165° C, kisha acha jiko lipate moto.

  Step2

  Chukua kikaango na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mafuta ya nazi, maple syrup, boga lililo sagwa, mdalasini, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2.

  Step3

  Weka vikombe 8 vya bisi zilizopikwa kwenye sufuria. Mimina mchanganyiko ulio ukaanga kwenye hilo sufuria lenye bisi, kisha changanya vizuri.

  Step4

  Weka sufuria hilo lenye bisi kwenye jiko la kuoka na uoke kwa muda wa dakika 6 mpaka 8. Kumbuka kukoroga bisi mara kwa mara, kila baada ya dakika 3.

  Step5

  Ukiona bisi zimeiva vizuri, ziondoe kutoka kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe. Weka vikombe 2 vya bisi vilivyobaki kwenye hilo sufuria, kisha changanya vizuri halafu acha zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.