-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji20
Biskuti za machungwa na mpopi, ni biskuti tamu zilizo sheheni ladha ya machungwa halisi pamoja na mbegu za mpopi. Biskuti hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida katika muda na wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za machungwa na mpopi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai na maganda ya machungwa, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, chumvi, baking powder pamoja na mbegu za mpopi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review