Jarida la Mapishi

Bisi za pilipili

Bisi za pilipili | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 5
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    10

Bisi za pilipili, ni bisi tamu ambazo hupikwa kwa kutumia pilipili ya unga pamoja na viungo vingine. Bisi hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida kwenye sherehe yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza bisi hizi za pilipili.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Washa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 150° C kisha acha jiko lipate moto.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hilo sufuria bisi pamoja na siagi, halafu changanya vizuri, kisha weka pembeni.

    Step3

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, vitunguu swaumu, limao, pilipili, vitunguu maji, pamoja na paprika, kisha changanya vizuri. Nyunyizia mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye bisi, kisha changanya vizuri.

    Step4

    Weka sufuria hilo lenye mchanganyiko wa bisi kwenye jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 5 mpaka 10.

    Step5

    Bisi zikisha iva, ziondoe kutoka kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe, kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.