Jarida la Mapishi

Mahindi ya viungo

Mahindi ya viungo | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Mahindi ya viungo, ni kitafunio kizuri na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mahindi mabichi yaliyo chemshwa, vitunguu maji, pilipili hoho, pamoja na viungo mbali mbali. Mahindi haya yanafaa kula kama kitafunio cha kawaida wakati wa mchana au wakati wa jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mahindi haya ya viungo.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mahindi kwenye hicho kikaango, kisha pika huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona maji maji yote yaliyomo kwenye mahindi yamekauka. Ondoa mahindi kwenye kikaango na uyaweke kwenye kontena.

    Step2

    Weka kwenye kikaango hicho hicho mafuta ya kupikia, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka mahindi, mbegu za uwatu, binzari nyembamba, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona mahindi yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Weka Tamarind Paste, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona maji maji ya Tamarind Paste yamekauka.

    Step5

    Weka pilipili hoho pamoja na majani ya giligilani, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.