-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Vimanda vya viungo, ni vitafunio vyenye ladha ya kipekee ambavyo hupikwa kwa kutumia mayai, vitunguu maji, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Vimanda hivi vyafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi pamoja na mkate au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika vimanda hivi vya viungo.
Ingredients
Directions
Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, mayai, chumvi, pamoja na pilipili manga, kisha piga piga vizuri mchanganyiko huo.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, majani ya giligilani, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena lenye mchanganyiko wa mayai, kisha changanya vizuri.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mchanganyiko wa mayai uliochanganya, kisha funika kikaango na ukaange kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona upande wa chini wa mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. (Weka mchanganyiko huo wa mayai kwa awamu 2 mpaka 3)
Chukua sahani kubwa. Weka sahani hiyo ndani ya kikaango, kisha pindua kikaango juu chini ili kimanda kipate kigeuka na kuhamia kwenye sahani.
Telezesha kimanda kwenye kikaango, halafu rudisha kikaango kwenye jiko, kisha kaanga upande wa pili wa kimanda hicho kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona na upande huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Kunja kimanda katikati, kisha ondoa kwenye kikaango na ukiweke kwenye sahani, tayari kwa kula. Rudia hatua ya 3 mpaka 6, kwa mchanganyiko wa vimanda uliobaki.
Leave a Review