-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji30
Kama wewe ni mpenzi wa biskuti, basi jaribu pishi hili la biskuti za maziwa. Huna haja ya kuwa na hofu endapo hujawahi kupika biskuti, kwa sababu biskuti hizi ni rahisi kupika na zina maelezo kina ya hatua kwa hatua ya namna ya kupika. Fuata maelekezo yafuatayo, ili kujifunza jinsi ya kupika biskuti hizi za maziwa.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, sukari, vanilla extract pamoja na lemon zest, kisha changanya vizuri.
Weka ute wa mayai pamoja maziwa na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, maziwa ya unga, baking powder na chumvi, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review