Jarida la Mapishi

Biskuti za tangawizi

 • Maandalizi
  Saa 1
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  20

Biskuti za tangawizi, ni mojawapo ya biskuti zinazopendwa zaidi nchini Uingereza, na zimekuwa zikiliwa nchini humo kwa karne nyingi. Biskuti hizi zafaa sana kuliwa pamoja na chai, ingawa pia waweza kula biskuti hizi pamoja na kinywaji chochote kile ukipendacho. Tangawizi iliyomo ndani ya biskuti hizi, husaidia kutibu maradhi mengi ya tumbo pamoja na kuongeza joto mwilini. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsj ya kupika biskuti hizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi na sukari, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona sukari imechanganyika vyema pamoja na siagi.

  Step2

  Weka yai na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, tangawizi, iliki, chumvi na baking soda, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Craymartin

   Safi sana hongera kwa darasa

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *