-
MaandaliziDakika 50
-
KupikaDakika 10
-
Walaji10
Biskuti za shayiri na ndizi, ni biskuti tamu na zenye afya ambazo hupikwa kwa kutumia ndizi mbivu zilizo katwa katwa, shayiri, pamoja na maple syrup. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jonsi ya kupika biskuti hizi za shayiri na ndizi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, ndizi, maple syrup, shayiri na baking soda, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review