Jarida la Mapishi

Biskuti za jozi na ndizi

Biskuti za jozi na ndizi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 46
  • Kupika
    Dakika 14
  • Walaji
    20

Biskuti za jozi na ndizi, ni biskuti tamu na rahisi kupika, ambazo hupikwa kwa kutumia ndizi mbivu, unga wa ngano, shayiri, pamoja na jozi mbichi. Biskuti hizi zafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Pia waweza kula biskuti hizi kama kitafunio cha kawaida katika muda na wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza biskuti hizi za jozi na ndizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na dark brown sugar, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka yai, vanilla extract na ndizi, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano ambao hauja kobolewa, unga wa ngano, chumvi, baking powder, dark chocolate chips, pamoja na jozi, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 14, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.