Jarida la Mapishi

Sambusa za nyama

Sambusa za nyama | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 2 Dk. 10
  • Walaji
    24

Sambusa za nyama, ni sambusa tamu ambazo hupikwa kwa kutumia nyama ya kusaga iliyo changanywa pamoja na viungo. Sambusa hizi zaweza kupikwa kwa kutumia nyama yoyote ile; iwe ni nyama ya ng'ombe, nyama ya mbuzi, au nyama ya kuku. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika sambusa hizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, majani ya uwatu, majani ya giligilani, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Weka kungumanga, binzari ya manjano, chembelele, ½ kijiko cha chai cha chumvi, nyama ya kusaga, pamoja na garam masala, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vizuri.

    Step3

    Chukua kikaango kikubwa na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mchanganyiko ulio usaga pamoja na njegere, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step4

    Chukua mashine ya kusaga (food processor). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vikombe 1½ vya unga wa ngano, baking powder, chumvi, baking soda, ¼ kikombe cha mafuta ya kupikia, mbegu za kisibiti, pamoja na kijiko 1 cha chai cha chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.

    Step5

    Mimina ⅓ ya kikombe cha maji taratibu wakati mashine ikiendelea kuzunguka, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umejikusanya na kuwa donge lenye umbo la mpira ambalo halishikamani na chombo. Ondoa donge hilo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uliweke kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo, kisha acha donge liumuke kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.

    Step6

    Chukua mafuta ya kupikia kiasi na uyapake kwenye viganja vya mikono yako. Chukua donge lililomo kwenye kontena, kisha ligawe katika madonge 12 ya maumbo ya mpira yenye uwiano unao fanana. Weka madonge hayo kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step7

    Chukua kibao cha kusukumia chapati. Chukua donge moja kutoka kwenye kontena na uliweke juu ya kibao cha kusukumia chapati, kisha kandamiza vizuri donge hilo kwa kutumia kiganja cha mkono wako hadi utakapo ona imekuwa bapa.

    Step8

    Chukua unga wa ngano na upake juu ya donge ulilo likandamiza. Chukua kifimbo cha kusukumia chapati, kisha sukuma hadi utakapopata chapati ya upana wa kati ya nchi 6 hadi 7. (Unaweza kupaka unga zaidi wakati unasukuma, ikiwa utaona donge hilo linanata)

    Step9

    Chukua kisu na ukate chapati hiyo katikati, kisha chukua maji na upake kwenye kingo za vipande hivyo vya chapati.

    Step10

    Chukua kipande kimoja cha chapati. Chukua upande mmoja wa kipande hicho cha chapati na ukunje katikati, halafu chukua na upande wa pili wa kipande hicho cha chapati na ukunje pia katikati ili kutengeneza umbo la koni. Hakikisha kingo za pande zote mbili za hiyo chapati zimekutana, kisha kandamiza kingo hizo ili ziweze kushikamana.

    Step11

    Fungua mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha weka ndani yake vijiko 2 hadi 3 vya chakula vya mchanganyiko wa sambusa ulio upika.

    Step12

    Chukua maji na upake kwenye kingo za mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha kandamiza kingo hizo, hadi utakapo ona mdomo wa sambusa umejifunga vizuri. Weka sambusa hiyo kwenye kontena safi, kisha funika vizuri kontena hilo, hadi utakapokuwa tayari kukaanga sambusa hizo. Rudia hatua ya 7 hadi ya 12 kwa madonge yaliyobaki.

    Step13

    Chukua kikaango kikubwa chenye vikombe 2 vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango sambusa ambazo zinatosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa sambusa hizo kutoka kwenye kikaango na uziweke kwenye kwenye chombo chenye paper towel ili zikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa sambusa nyingine zote zilizobaki.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Recipe Reviews

    • Lizzy

      I like it

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.