-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji20
Biskuti za kahawa, ni biskuti rahisi kupika ambazo zinaweza kufurahiwa na mtu yoyote, hasa wapenzi wa kahawa. Biskuti hizi zinapikwa kwa kutumia mahitaji rahisi ambayo tayari unayo nyumbani kwako, kama vile kahawa, unga wa ngano, chumvi, siagi, baking powder pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kuoka biskuti hizi za kahawa.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, mafuta ya nazi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona sukari imechanganyika vyema pamoja na siagi na mafuta ya nazi.
Weka yai pamoja na vanilla extract na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, baking soda, chumvi, mdalasini, tangawizi, iliki, na kahawa, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review