Jarida la Mapishi

Bisi za vitunguu swaumu na cheese

 • Maandalizi
  Dakika 5
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  8

Bisi za vitunguu swaumu na cheese, ni bisi rahisi kupika zenye ladha ya vitunguu swaumu, ambazo hupikwa kwa kutumia vitunguu swaumu vya unga. Bisi hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida, iwe ni kwenye sherehe, filamu, michezo au wakati wowote ule upendao. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bisi hizi za vitunguu swaumu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka bisi zilizopikwa ndani ya hilo bakuli, kisha weka pembeni.

  Step2

  Chukua kikaango kidogo chenye siagi na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi iyeyuke. Weka vitunguu swaumu kwenye hicho kikaango, kisha kaanga kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Epua mchanganyiko huo wa vitunguu swaumu na siagi na umimine kwenye bakuli lenye bisi. Weka pia kwenye hilo bakuli, cheese pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri, halafu acha bisi zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *