-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji20
Biskuti za pistachio na machungwa, ni biskuti zinazopikwa kwa kutumia machungwa yaliyo kamuliwa, maganda ya machungwa yaliyokunwa, pamoja na pistachio zilizo katwa katwa. Biskuti hizi zafaa sana kula katika msimu wa sikukuu za krismasi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za pistachio na machungwa.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, pistachio, unga wa ngano, chumvi, baking powder, iliki, pamoja na mdalasini, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Weka mayai, maziwa, na maganda ya limao, halafu endelea kuchanganya.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review