-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji4
Bisi za mdalasini, ni bisi ambazo hupikwa kwa kutumia siagi iliyo yeyushwa, sukari, pamoja na mdalasini. Ladha ya bisi hizi, hufanya watoto wazipende zaidi. Waweza kula bisi hizi kama kitafunio cha kawaida katika muda na wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza bisi hizi za mdalasini.
Ingredients
Directions
Step1
Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli sukari pamoja na mdalasini halafu changanya vizuri, kisha weka pembeni.
Step2
Chukua bakuli kubwa. Weka bisi ndani ya hilo bakuli, halafu nyunyizia siagi juu ya hizo bisi, kisha changanya vizuri.
Step3
Nyunyinyizia mchanganyiko wa sukari juu ya bisi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review