Jarida la Mapishi

Bisi za chumvi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  8

Bisi za chumvi, kama jina lake lilivyo, ni bisi zinazopikwa kwa kutumia mafuta pamoja na chumvi. Bisi hizi ni rahisi sana kupika, na unaweza kuzipika kwa muda mfupi wa ndani ya dakika 10 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bisi hizi za chumvi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya nazi na uliweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mahindi ya bisi kwenye hilo sufuria, kisha pika mahindi hayo huku ukizungusha na kutikisa sufuria ili mahindi yote yaenee mafuta, lakini pia ili mahindi yasiungue.

  Step2

  Ukiona mahindi yanaanza kupasuka na kuwa bisi, funika sufuria, halafu endelea kupika huku ukitikisa sufuria hadi utakaposikia kasi ya kupasuka mahindi na kuwa bisi imepungua sana.

  Step3

  Fungua mfuniko wa sufuria, halafu weka mafuta ya nazi pamoja na chumvi, juu ya hizo bisi, kisha changanya vizuri.

  Step4

  Epua bisi hizo na uziweke pembeni ili zipoe, kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Meple

   Nice😋

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *